Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Featured Posts

Tuesday, October 25, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AMKARIBISHA MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, MIKATABA 21 YA USHIRIKIANO YASAINIWA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakilakiwa na wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakipigiwa  ngoma pamoja na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI  mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI  pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa  Ikulu jijini Dar es Salaam kushuhudia uwekaji saini Mikataba ya ushirikiano 21 kati ya nchi hizo mbili.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI  pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa  Ikulu jijini Dar es Salaam kushuhudia uwekaji saini Mikataba ya ushirikiano 21 kati ya nchi hizo mbili.

UN YAADHIMISHA MIAKA 71, YAAHIDI KUWEZESHA VIJANA

WAKATI Umoja wa Mataifa (UN) ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, imeahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo.

Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.

"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," amesema.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwenye sherehe ya kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya umoja huo ambapo kila mwaka Oktoba 24 huadhimishwa.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu ya umoja huo na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.

Aidha, Rodriguez amesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linasababisha umasikini kwa kuwa nguvu kazi hiyo inashindwa kuwajibika katika kuliletea taifa maendeleo.

AJALI ZA BARABARANI ZAENDELEA KUUA NA KUACHA MAJERUHI MKOANI MWANZA.

Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika ili kutokomeza ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3

Pichani juu ni maandamano ya bodaboda pamoja na wa watumiaji wengine wa barabara yakiingia Uwanjani kwenye maadhimisho hayo ambayo yamezinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza

MAHAKAMA YA RUFAA YASHIDWA KUTOA UKUMU KESI YA UCHAGUZI INAYOWAKIBILI ONESMO NANGOLE NA DKT KIRUSWA

mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya  maamuzi ya ruf
aa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la longine Onesmo Nangole
Na Woinde Shizza,Arusha 

Mahakama ya rufaa kanda ya Arusha imeshindwa kutoa maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa  na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido ,Onesmo Nangole(CHADEMA) ambaye anapinga maamuzi ya mahakama kuu iliyomvua ubunge wake, badala yake imeagiza mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo aunganishwe katika shauri hilo.

Aidha mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa mrufani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya notisi yake ya rufaa na kuyaleta mahakamani hapo ili msimamizi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali waingizwe  kama mashaidi  muhimu katika rufaa.

Akisoma taarifa ya majaji watatu walikuwa wakisikiliza rufaa hiyo mahakamani hapo Msajili wa mahakama rufaa John Kayanza alisema kuwa mahakama ya rufaa aitatenda haki katika hukumu yake iwapo haita msikiliza mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido na imewataja kama mashaidi muhimu kwa upande wa mrufani

WATANGAZAJI WA LAKE FM MWANZA KUTAMBULISHWA KWA WANANZENGO KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA KOPA

Usisahau kuhusu Show ya Usiku wa Mshike Mshike na Mfalme wa taarabu Afrka Mashariki na Kati iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.

Ni alhamisi wiki hii tarehe 27.10.2016 ndani ya kiwanja cha nyumbani, Villa Park Resort, kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi 10,000 baada ya saa tano usiku.

WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai. 

Saturday, October 22, 2016

PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, IKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI


 Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Dar es Salaam.
 Mwonekano wa pikipiki hiyo kwa nyuma.
Pikipiki hiyo ikiwa katika kijiwe hicho cha  Veterinary Maganga Temeke jijini Dar es Salaam.

MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MBALONI KWA KUDAIWA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake   kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA

 Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya  kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo

MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT MITO YA BARAKA JIJINI DAR ES SALAAM AHUDUMU KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Mchungaji  Bruno Mwakibolwa kutoka Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Temeke Jijini Dar es salaam, jumapili iliyopita Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika kanisa hilo akitokea nchini Kenya.

Ilikuwa Ibada iliyojaa neema ambapo Mchungaji Mwakibolwa aliwahimiza waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kumtumia Mungu kwa moyo wa kweli na watabarikiwa maishani mwao.

Alisema ziko njia mbalimbali za kumtumikia Mungu ikiwemo kuhakikisha waumini wanajikita katika kumjengea Mungu Makanisa bora ili kuwezesha neno la Mungu kusonga mbele.
Na BMG
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza